Tuesday, July 5, 2011

Simba yaitafuna Banamwaya yaingia nusu fainali

Kucheza na Al Mereikh ya Sudan

Timu ya Simba ya Tanzania leo imeingia hatua nusu fainali baada ya kuifunga timu ya Bunamwaya ya Uganda kwa jumla ya magoli 2 - 1 katika mchezo wa kwanza robo fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup  uliochezwa katika uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Tanzania.


Mshambuliaji wa Simba Muhamed Banka akijaribu kuwatoka mabeki wa Bunamwaya ya Uganda katika mechi ya robo fainali Kagame Cup
Katika mchezo mwingine wa robo fainali timu ya Al Mereikh ya Sudan imeifunga Ulinzi ya Kenya kwa njia ya mikwaju ya penati 9 - 8 , baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya goli 1 - 1.

Kwa matokeo hayo Simba ya Tanzania sasa itakutana na Al Mereikh ya Sudan katika mchezo wa nusu fainali utakapigwa siku ya katika uwanja huo wa Taifa wa Dar es Salaam Ijumaa wiki hii.

Leo jumatano katika uwanja huo huo wa Taifa wa Dar es Salaam kutakuwa na mchezo mwingine wa robo fainali  ambapo St. George ya Ethiopia itapambana na Vital'o ya Burundi huku Yanga ya Tanzania itakuwa na kibarua kigumu pale itakakutana na Red Sea ya Eritrea  katika mchezo wa pili wa robo fainali.

Haruna Moshi Boban wa Simba (mwenye jezi nyeupe) akipambana vikali na mmoja wa wachezaji wa timu ya Bunamwaya ya Uganda 

No comments:

Post a Comment