Sunday, July 10, 2011

Yanga Yatwaa kombe la Kagame mwaka 2011

 Yaisambaratisha Simba 1 - 0.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakifurahia baada ya kukabidhiwa kombe la Kagame
Timu ya Yanga ya Tanzania imelitwa Kombe la Kagame kwa mwaka 2011 baada ya mahasimu wao kisoka timu ya Simba pia ya Tanzania kwa goli 1 - 0 katika mchezo wa fainali wa kukata na shoka wa klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati uliofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Tanzania.

.Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake. Hivyo ikalazimu kuongezewa dakika 30 za nyongeza na ndipo katika dakika ya 109 Keneth Asamoah wa Yanga akafanikiwa kupachika goli zuri baada kupata pasi kutoka kwa Rashid Gumbo.


Kwa matokeo hayo Yanga ya Tanzania wanakuwa mabingwa wa Kombe CECAFA kwa upande wa vilabu Kagame Cup kwa 2011 na hivyo kuondoka na kitita cha dola za kimarekani 30,000.

Mshindi wa pili ambaye ni timu ya Simba amepata dola 20,000

Awali katika mechi ya kutafuta mchindi wa tatu wa mashindano hayo timu ya Al Mereikh ya Sudan iliifunga St. George ya Ethiopia magoli 2 - 0 na hivyo kuwa mshindi wa tatu wa michuano hiyo ambayo nayo imejinyakulia dola 10,000.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kuifunga Simba na kutwaa kombe la Kagame

 


 
Mashabiki wa Yanga


 

Mashaki wa Yanga wakitaniana na wa Simba muda mfupi kabla ya mpira kuanza

Wachezaji wa kisalimiana muda mfupi kabla ya mpira kuanza


Wanazi wa Simba






No comments:

Post a Comment