Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kupata bao |
Mshambuliaji wa Yanga Didier Kavumbagu akijaribu kuwatoka mabeki ya Azam na baadae kufunga bao |
Timu
ya Simba imepoteza mchezo wake wa kwanza tangu ligi Kuu ya Tanzania
bara ilipoanza msimu huu baada ya kukubali kipigo cha magoli 2 - 0
kutoka kwa wakata miwa wa Mtibwa timu ya Mtibwa Sugar..
Wakati
Simba kipata kipigo hicho wenzao Yanga walitamba Ice cream almaaruf
(shikirimu ) za Azam pale ilipoibanjua kwa jumla ya magoli 2 - 0 katika
mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo Yanga sasa imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambapo
imefikisha pointi 26, na kuizidi Simba ambayo sasa ina pointi 23 na kushika nafasi ya Pili.
Simba itamaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kwa kumenyana na
Toto African uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment