Saturday, November 10, 2012

Man U yaishushia kipigo Aston Villa 3 -2

Chicharito wa Man mfungaji wa magoli yote matatu akiondoka na mpira wake jana ambapo  Man iliichabanga Aston Villa 3 - 2

Toto Africa yaikandamiza Simba 1 - 0

Bao pekee la Mussa Said Kimbu dakika ya 73, leo limeizamisha Simba SC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kimbu alifunga bao hilo akiunganisha krosi ya Mganda, Mohamed Jingo tena akipitisha mpira katikati ya msitu wa mabeki wa Simba na kipa wao, Wilbert Mweta.
Katika michezo mingine ya ligi hiyo, Azam imefungwa 2-1 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwa matokeo hayo, Yanga inazidi kujinafasi kileleni kwa pointi zake 26, baada ya kucheza mechi 12 na kesho itahitimisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kwa kucheza Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Simba inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 23 na Azam yenye pointi 24 ni ya pili.

Wednesday, November 7, 2012

Matoke Mechi za UEFA Champions League haya hapa





Bayern Munich         6 - 1      Lille           
Benfica                    2 - 0   Spartak Moscow     
Braga                      1 - 3     Man Utd                    
Celtic                      2 - 1    Barcelona               
CFR Cluj-Napoca   1 - 3    Galatasaray 
Chelsea                   3 - 2    Shakhtar Donetsk     
Juventus                  4 - 0    Nordsjaelland 
Valencia                   4 - 2    BATE Borisov





























Sunday, November 4, 2012

Mtibwa yaitafuna Simba 2 -0, Yanga yailamba Azam 2 - 0


Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kupata bao
Mshambuliaji wa Yanga Didier Kavumbagu akijaribu kuwatoka mabeki ya Azam na baadae kufunga bao
 Timu ya Simba imepoteza mchezo wake wa kwanza tangu ligi  Kuu ya Tanzania bara ilipoanza msimu huu baada ya kukubali kipigo cha magoli 2 - 0 kutoka kwa wakata miwa wa Mtibwa timu ya Mtibwa Sugar..

Wakati Simba kipata kipigo hicho wenzao Yanga walitamba Ice cream almaaruf (shikirimu ) za  Azam pale ilipoibanjua kwa jumla ya magoli 2 - 0 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo Yanga sasa imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambapo
 imefikisha pointi 26, na kuizidi Simba ambayo sasa ina pointi  23 na kushika nafasi ya Pili.
Simba itamaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kwa kumenyana na Toto African uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Tuesday, October 30, 2012

Mtanzania apigwa kwa Technical Know out Afghanstan

Habari ambazo zimetufikia hivi punde mpambano baina ya  bondia wa Afghanstan Hamid Rahimi na mtanzania, Said Mbelwa limemalizika kwa Said Mbelwa kushindwa kuendelea baada ya kuumia bega na hivyo Hamid Ramimi kuwapewa ushindi wa technical  knock out.

Pambalo hilo ambalo lilikuwa likufuatiliwa sehemu mbali mbali ilikuwa lilipewa jina la "Pambano la Amani".

Saturday, December 10, 2011

Uganda Mabingwa wa CECAFA 2011



Wachezaji wa timu ya taifa ya Uganda the Cranes wakifurahia na kombe la ubingwa wa CECAFA

 Timu ya Uganda umenyakua ubingwa wa Michuano ya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP mwaka 2011 baada ya kuifunga timu ya Rwanda katika mchezo wa fainali ulichezwa katika uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam Tanzania.

Uganda imeifunga timu ya Rwanda kwa penati 3 -2 baada ya kumaliza dakika 90 za kawaida zikiwa zimefungana 2 -2 ambapo ziliongwezwa dakika 30 ambazo nazo hazikuweza kumtoa mshindi.

Kipa wa Uganda Abby Dhaira ndiye aliyedaka penati ya mwisho ya Rwanda iliyopigwa na Ngabo Albert baada kumaliza ikiwa imepata penati 3 na kukosa 2. Rwanda ilipata penati 2 na kukosa 3.



Nahodha wa Uganda Cranes akipokea kombe la CECAFA kutoka kwa mgeni Rasmi  Rais wa Zanzibar Dr. Alli Mohamed Shein



Nahodha wa Uganda Cranes Andrew Mwesigwa


 Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) na Sudan, timu ya Sudan imeifunga Tanzania bara 1 - 0 na kunyakuwa nafasi ya tatu.

Kwa matokeo hayo timu ya Taifa ya Uganda ambao wamenyakua Ubingwa imepata kombe pamoja na kitita cha Dola za kimarekani 30,000 ambapo mshindi wa pili ambaye ni Rwanda imepewa dola 20,000 wakati mshindi wa tatu Sudan imenyakua dola 10,000.