Wednesday, July 6, 2011

Leo Yanga kufa na kupona Kagame Cup


Kikosi cha timu ya Yanga ya Tanzania

Leo timu ya Yanga ya Tanzania inaingia uwanjani kumenyana na timu na Red Sea ya Eritrea katika mechi ya inayotarajiwa kuwa ya kukata na shoka ya robo fainali ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup katika uwanja wa Taifa wa Dar es Saam.

Katika mechi nyingine ya robo fainali itakayopigwa majira ya saa 8 za mchana katika uwanja huo huo timu ya St. George ya Ethiopia itamenyana vikali na Vital'o ya Burundi katika mechi nyingine inayotariwa kuwa ya kuvutia.

Tayari timu za Simba ya Tanzania na Al Mereikh ya Sudan zimeshaingia hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ya CECAFA Kagame Cup.

Simba imeingia nusu fainali baada ya kuifunga Bunamwaya ya Uganda kwa magoli 2 - 1.  Na El Mereikh imeingia nusu fainali baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati timu ya Ulinzi ya Kenye kwa penati 9 -8.

No comments:

Post a Comment