Sunday, July 3, 2011

Simba yabanwa, Ocean View hoi Kagame Cup

Timu ya Simba ya Tanzania imeshindwa kutamba mbele ya Red Sea ya Eritrea katika mechi ya mwisho ya kundi A kumalizia hatua ya makundi ya michuano ya Kagame Cu uliofanyika katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam Tanzania.

Hadi mchezo unamalizika matokeo yalikuwa 0 - 0.



Ulimboka Mwakingwa wa Simba (kulia) akijaribu kumpita mmoja wa mabeki wa Red Sea ya Eritrea
Nayo Zanzibar Ocean View imekubali kipigo cha goli 1 - 0 kutoka kwa  Vital'o ya Burundi na hivyo kuondolewa katika mashindano hayo.

Goli la Vital'o lilipatikana kwa njia penati katika kipindi cha kwanza ambapo hadi mpira unamalizika matokeo yalikuwa 1 - 0.

No comments:

Post a Comment