Saturday, July 9, 2011

Yale yaleeee Simba vs Yanga fainali Kagame Cup

Ni baada ya Yanga kuifunga kwa penati St. George


Wachezaji wa Yanga wakifurahia baada ya timu kuingia fainali
Timu ya Yanga imeingia fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup baaada ya kuisambaratisha timu ya St. George ya Ethiopia kwa njia ya mikwaju 5 - 4 katika mechi ya kukata na shoka ya nusu fainali iliyochezwa katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam, Tanzania.

Timu hizo zimefikia hatua ya kupigiana penati baada ya dakika 90 na hatimaye 30 za nyongeza kutompata mshindi.

Kwa matokeo hayo sasa Yanga ya Tanzania itacheza fainali na Simba nayo ya Tanzania siku ya Jumapili. Simba iliingia fainali baada ya kuiondoa Al Mereikh ya Sudan kwa mtindo huo huo wa mikwaju ya penati kwani nazo ilibidi zicheze dakika 120 lakini hata hivyo hadi mwisho zilikuwa zimefungana 1 - 1.

St. George ya Ethiopia na Al Mereikh ya Sudan zitakutana katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano hayo itayochezwa mapema siku ya jumapili kabla ya mechi ya fainali.

Bingwa wa Kombe la Kagame atazawadiwa dola za kimarekani 30,000 ambazo zimetolewa na rais Rwanda Paul Kagame.

Godfrey Taita wa Yanga akishindana na mmoja wa wachezaji wa St. George

Nurdin Bakari wa Yanga akipambana na mmoja wa wachezaji wa St. George

No comments:

Post a Comment