Thursday, July 7, 2011

Simba yaingia fainali Kagame Cup kwa kishindo


Yaiadhibu Al Mereikh ya Sudan
Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kuingia fainali Kagame Cup

Simba ya Tanzania imetinga fainali Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup, mwaka 2011 baada ya kuiadhibu timu ya Al Mereikh ya Sudan kwa mikwaju ya penati 5 - 4 katika mechi ya kusisimua iliyochezwa katika uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Ni Mlinda Juma Kaseja wa Simba ambaye ndiye aliyeidaka penati ya mwisho iliyopigwa na Al Mereikh na hivyo kuifanya timu yake kutinga moja kwa moja fainali.

Mechi hiyo ilibidi kuamuliwa na mikwaju ya penati baada ya mchezo huo kumalizika dakika 90 bila kupatikana mshindi na hata walipoongezewa dakika 30 za nyongeza hazikuzaa matunnda  kwani hadi mwisho wa dakika 120 walikuwa wamefungana 1 -1.

Patrick Masango akimbeba Juma Kaseja baada ya kuokoa penati ya mwisho

Simba itacheza fainali Siku ya jumapili na timu itakayoshinda katika mechi ya nusu fainali kati ya Yanga ya Tanzania na St.George ya Ethiopia itakayochezwa siku ya Ijumaa.

Mechi ya Simba na Al Mereikh katika picha:

Mlinda mlango wa Simba Juma Kaseja akisindikizwa na mmoja wa mashabiki wa Simba

Amiri Maftah kushoto  akicheza na Juma Kaseja pamoja na mpenzi wa mmoja wa Simba


No comments:

Post a Comment