Wednesday, July 6, 2011

Simba leo kufia uwanjani nusu fainali Kagame Cup


Kikosi cha Simba ya Tanzania
Timu ya Simba ya Tanzania leo inaingia katiika mechi ya nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup kupambana na Al Mereikh ya Sudan katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam Tanzania mechi inayotarajiwa kuwa ya kuvutia kufuatia historia ya timu zote mbili.

Simba itaingia uwanjani ikiwategemea zaidi mashabiki wake wanaotarijiwa kumiminika kwa wingi katika uwanja huo huku ikizingatiwa simba watakuwa wapo nyumbani.

Timu ya Al Mereikh ya Sudan


Musa Hassan Mgosi, Haruman Moshi Boban, Muhamed Banka na Ulimboka Mwakingwe wanatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji huku Patric Mafisango , Jerry Santo , Amiri Maftah ,Athumani Idd Chuji wakitarajiwa kusimama katika nafasi ya kiungo wakati safu ulinzi ikitarajiwa kuongozwa na Walulya Derrick, Juma Nyoso na Kevin Yondan.

No comments:

Post a Comment